Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi na wanachama wake kuwa na subira kwa imejipanga kufanya usajili wa maana dirisha dogo, imeelezwa.
Yanga imeamua kuvunja ukimya kutokana na kuanza kupokea malalamiko juu ya viwango vya baadhi ya wachezaji wake ambao inawategemea kwa sasa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema kuwa kwa sasa uongozi unajipanga kuhakikisha inakuja kufanya usajili pindi dirisha likapofunguliwa.
Hatua hii imekuja mara baada ya wanayanga kadhaa kuwatupia lawama wachezaji ikiwemo Heritier Makambo ambaye wameanza kumuona kama ana mapungufu uwanjani.
Dirisha la usajili litafunguliwa Novemba 15 mwezi huu na tayari baadhi ya timu zimeshaanza kuingia mikataba ya awali ikiwemo Azam FC baada ya kumalizana na Obrey Chirwa aliyewahi kuichezea Yanga.
0 comments:
Post a Comment