Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema timu hiyo inakusudia kucheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kwenda mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui Fc Novemba 22 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Baada ya mchezo dhidi ya African Lyon utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Uhuru, siku ya jumatano Yanga inatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu kutoka nchini Malawi.
Kaya amesema Novemba 17 Yanga itasafiri kwenda mkoani Lindi kuikabili Namungo Fc kwenye mchezo mwingine wa kirafiki utakaopigwa kwenye uwanja wa Majaliwa, wilayani Ruangwa
0 comments:
Post a Comment