Wednesday, November 7, 2018

Ofisi ya mwendesha mashtaka katika mji wa Rio Grande Do Sul nchini Brazil imeagiza kuzuiwa kwa hati ya kusafiria (passport) na kufungia akaunti za fedha za Ronaldinho Gaucho.

Lakini jambo la kushangaza ni pale mamlaka za kisheria zilipokuta kiasi cha dola 6 tu za kimarekani katika akaunti zote za Ronaldinho. Fedha hizo ni sawa na Shilingi 13, 740 za Kitanzania.

Kwa sasa Ronaldinho hayupo nchini Brazil na kwa hivyo hati yake ya kusafiria haijaweza kuzuiwa.

Mahakama imeagiza azuiwe mara moja atakapoingia nchini humo, na kuongeza kuwa maisha ya Mwanasoka huyo nguli hayafanani na kiasi cha fedha kilichokutwa katika akaunti zake za benki.

Tangu mwaka 2015, Ronaldinho anadaiwa faini ya Dola Milioni 2 za kimarekani baada ya kukutwa na hatia ya kujenga kiwanda cha sukari katika eneo la hifadhi ya Taifa huko Brazil, lakini hakuwahi kulipa kiasi chochote cha fedha.

0 comments:

Post a Comment