Aliyekuwa raisi wa shirikisho la soka nchini Ghana Football Association (GFA) Kwesi Nyantakyi amefungiwa maisha kutokujihusisha na soka.
FIFA walifanya uchunguzi wa kina kujua kama kweli alihusika katika sakata hilo la kupokea kiasi cha $65,000 (£48,000) kutoka kwa mwandishi wa habari aliyetumwa maalumu kwa ajili ya kupima uaminifu wa raisi huyo.
Fifa walimpiga Nyantakyi faini ya £390,000.
Nyantakyi aliwahi kuwa makamu wa Confederation of African Football na mjumbe wa halmashauri kuu ya Fifa.
Aliachia uraisi wa GFA mwezi June baada ya kugundulika kupokea malipo hayo. Fedha hizo alizipokea kitoka kwa mwandishi wa shirika la habari la nchini Uingereza Anas Aremeyaw Anas.
Nyantakyi baadae alijiondoa kwenye nyadhifa zake za Caf na Fifa. Ingawa Raisi huyo alikanusha kuwa hakupokea kiasi hicho kwa lengo la rushwa, ila baadhi ya watu wenye chuki zao binafsi waliamua kumtengenezea mazingira hayo. Hata hivyo aliomba radhi kwa raisi wa Ghana na wananchi wote kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment