Thursday, November 15, 2018

Jana Wyne Rooney amestaafu rasmi kuitumikia timu ya taifa ya uingereza akowa ameitumikia katika michezo 120 nakufanikiwa kufunga magoli 53.

Rooney alianza maisha yake ya soka katika klabu ya everton toka utotoni , akasajiliwa na manchester united huko ndiko  maajabu yake yalikoanzia.

Alicheza sana kama kiungo mshambuliaji, alikuwa ana kasi , anafunga magoli katika hali yoyote ile. Akiwa na machester amecheza fainali mbili za UEFa champions ligi na kufanikiwa kuchukua mara moja.

Pamoja na mafanikio yote hayo huoni Rooney akisemwa sana kiufundi wa soka, lakini atazungumziwa sana kwa utukutu wake ikiwemo ulevi, umalaya na vurugu vurugu zake.

Wamesahau kama ndiye mfungaji bora wa  mda wote kwa ngazi zote klabu na timu ya taifa. Tena akiwa kama kiungo.

 Amefunga magoli 253 akiwa na mashetani wekundu. Akimpiku Bob chalton mwenye magoli 247.

Kwa sasa wyne rooney anacheza soka la kulipwa nchini marekani katika klabu ya DC United. Na ameapa atastaafia soka kule.

0 comments:

Post a Comment