Hatimaye uongozi wa Yanga umekubali kutekeleza agizo la Shirikisho la Soka nchini TFF la kufanya uchaguzi wake tarehe 13, Januari 2019 kwaajili ya kuziba nafasi mbalimbali kama ilivyoelekezwa na Baraza la Michezo (BMT).
Katika mkutano na wanahabari uliojumuisha viongozi wa Yanga na TFF, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Thobias Lingalangala amesema nafasi zitakazogombewa kwenye uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne waliojiuzulu mwaka huu.
Amesema fomu zimeanza kutolewa leo Novemba 9 na gharama yake ni shilingi 200,000 kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyeki, huku nafasi ya ujumbe gharama ya fomu ikiwa ni shilingi 100,000.
Lingalangala ambaye ametambulishwa rasmi leo kukaimu nafasi ya Mwenyekiti iliyoachwa na Yusuph Manji, amewaonya baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kuacha vitendo vinavyoweza kukwamisha uchaguzi huo.
Amesisitiza “Akitokea mwanachama yeyote anayetaka kufanya kitu cha ajabu, mimi nitamkabidhi TFF washughulike naye”.
0 comments:
Post a Comment