Mshambuliaji wa klabu ya Coastal Union Ali Salehe Kiba amefanya mabadiliko kwenye mkataba wake na klabu ya Coastal Union ya Tanga. Mwanzo wa msimu huu Alikiba alisaini mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu ya Coastal Union ambao alitakiwa kulipwa mshahara wa milioni 10 kwa mwezi.
Klabu ya Coastal Union imeshindwa kuulipa mshahara huo ndio wakakaa meza moja na Alikiba ambaye pia ni mdhamini wa klabu hiyo kwa asilimia 40 kwa kinywaji cha Mo Faya pande zote mbili zimekubaliana Alikiba kuwa asilipwe mshahara wowote na awe na uhuru wa kuamua kucheza mechi au laah bila kupangiwa na mtu, kocha au uongozi wa klabu hiyo.
Pia Alikiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa klabu hiyo na sasa atafanya kazi Coastal Union kama kiongozi na si Mchezaji ila akiamua kucheza ni uamuzi wake. Mkataba wa udhamini wa Mo Faya na Coastal ulikuwa kutoa milioni 80 kwa msimu na sasa tayari Alikiba ametoa milioni 40 za Mwanzo na milioni 40 zilizobaki hazitatolewa kutokana na klabu ya Coastal kushindwa kumlipa mshahara kwa miezi minne.
0 comments:
Post a Comment