Draw ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika (Caf Champions League) itafanyika Cairo Misri siku ya Ijumaa December 28 na klabu ya Simba itawakilishwa na mwenyekiti wa bodi Swed Kwabi.
-Shirikisho hilo limepanga pot 4 kila pot ina timu 4 na kila pot itatoa timu moja kwenye kundi moja. Pot hizo zimepangwa kulingana na Parfomance ya klabu kwa miaka mitano iliyopita kwa Caf Champions League na Caf Confederation Cup.
-Pot 1 ina vilabu vya TP Mazembe (DR Congo) yenye pointi 66, Al Ahly (Egypt) yenye pointi 62, Wydad Casablanca (Morocco) yenye pointi 51 na Esperance de Tunis (Tunisia) yenye pointi 45.
-Pot 2 ina vilabu vya Mamelodi Sundowns (South Africa) yenye pointi 40, AS Vita Club (DR Congo) yenye pointi 29, Horoya (Guinea) yenye pointi 19 na Club African (Tunisia) yenye pointi 12.
-Pot 3 ina vilabu vya ASEC Mimosas (Ivory Coast) yenye Point 8.5, Orlando Pirates (South Africa) yenye pointi 8, FC Constantine (Algeria) na FC Platinum (Zimbabwe) zenye pointi 0
-Pot 4 ina vilabu vya Simba SC (Tanzania), Lobi Stars (Nigeria), Ismaily (Egypt), JS Saoura (Algeria) zote Zikiwa na Pointi 0
-Kila Pot itatoa timu moja kwa kila kundi, timu ambazo zipo pot moja haziwezi kupangwa kundi moja. Mechi za makundi zitaanza January hadi March kutakuwa na makundi manne yenye timu nne na kila timu itacheza mechi 6 ikiwa mechi 3 za nyumbani na mechi 3 za ugenini.
-Mechi za kwanza kwenye kundi zitapigwa January 11-13, mechi ya pili kwenye kundi zitachezwa January 18-20 mechi za tatu zitachezwa February 1-3 wakati mechi za nne zitachezaa February 12-13 mechi za tano kwenye kundi zitachezwa March 8-11 na mechi za mwisho kwenye kundi zitachezwa March 15-18.
-Timu mbili ambazo zimemaliza nafasi ya juu kwenye kila kundi zitafuzu kucheza robo fainali ya Caf Champions League na draw ya Robo fainali na nusu fainali itafanyika Cairo Misri March 23. Wakati mechi za Robo fainali zitachezwa April 5-7, nusu fainali April 26-28 na fainali ni May 24-25.
0 comments:
Post a Comment