Friday, December 14, 2018

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limekili kutoipatia Mtibwa Sugar fedha za ubingwa wa michuano ya Azam Sports Federation,

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari Leo katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema kwamba fedha zimeshindwa kutolewa kwa wakati kutokana na makubaliano yao na mdhamini mkuu wa michuano hiyo hasa katika taratibu za mgawanyo wa fedha kwa vilabu husika.

Kidao amesema kwamba hata klabu ya Simba haijapewa fedha zake za ubingwa wa michuano hiyo ya FA kutokana na sababu mbalimbali ambazo TFf na Azam wanazifahamu.

0 comments:

Post a Comment