Friday, December 14, 2018

Mwanachama wa klabu ya soka ya Yanga,Spriani Msiba amemlipa kiasi cha shilingi milioni 2 mlinda mlango wa timu hiyo Beno Kakolanya ikiwa ni fedha za usajili ambazo alikuwa anaidai klabu hiyo.

Akizungumzia mbele ya waandishi wa Habari wakati akikabidhi fedha hizo Msiba amesema kuwa Kakolanya amekuwa akiidai klabu hiyo kiasi cha shilingi milioni 15 ambazo ni fedha za usajili.

Amesema kwamba kiasi ambacho kimesalia cha milioni 13 atazilipa yeye mwenyewe kwa utaratibu maalumu.

0 comments:

Post a Comment