Monday, June 4, 2018

Kaimu mwenyekiti wa klabu ya yanga amezungumza mengi alipo fanya mahojiano na kipindi cha clouds tv na redio sports extra. Aligusia hasa maisha ya Yanga baada na kabla ya manji hajastaafu kuitumikia club hiyo.

“Tulikuwa na kipindi cha neema kipindi hicho Manji yupo. Alikuwa analipa mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wengine kwa kiasi kisichopungua Tsh. 125M kwa mwezi.

“Masuala ya usajili kwa wastani tulikuwa tunaweza kusajili wachezaji kwa kiasi cha Tsh. 500 hadi 600M.

“Kwa hiyo unaweza kuona ni gap kubwa kwa yeye kutokuwepo ndani ya uongozi na kama mfadhili wa klabu ya Yanga.
Alipotangaza kujiuzulu ilikuwa kama mshtuko  na katika hali ya kawaida huwezi kutafuta njia ya kukimbia badala yake unajipanga na kutulia ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Tunashirikiana na kamati ya utendaji kwa pamoja na mazingira yaliyopo, tangu Manji ameondoka tulikuwa na deni kama miezi mitatu mapaka leo ni wastani wa miezi 18 ambayo pia nimekuwa nikikaimu nafasi yake.

“Katika miezi hiyo 18 uongozi huu uliobaki umeweza kulipa mishahara kwa miezi 16, tuna deni la mishahara ya miezi miwili ambalo tunaendelea kulifanyia kazi kuhakikisha tunakamilisha. Changamoto ni moja, kwamba mishahara ilikuwa haiji kwa wakati katika kipindi chetu lakini kwa kifupi tuna deni la mishahara ya miezi 2"

Miongoni mwa mambo ambayo aliyadadavua upana ni maisha ya Yanga kabla na baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji.

“Tunashukuru kwa alichofanya Manji katika kipindi chote ambacho alikuwa madarakani na kabla ya kuwa madarakani wakati huo akiwa mdhamini wa klabu, amekuwa ni msaada mkubwa.
Kila mwanachama na mpenzi wa Yanga anajua maisha tuliyokuwa nayo wakati huo, Manji alikuwa mpiganaji na timu iliweza kufanya vizuri kwa kipindi chote ambacho alikuwepo.

“Katika kipindi cha hivi karibuni wakati Manji yupo Yanga tuliweza kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kambi mbalimbali hakukuwa na tatizo la kulipa mishara, ilikuwa inalipwa kwa wakati.
Aina ya wachezaji na benchi la ufundi lilikuwa ni zuri sana katika vipindi vyote ambavyo alikuwepo na hakukuwa na dosari.”

0 comments:

Post a Comment