Sunday, September 16, 2018

Hatimaye Cristiano Ronaldo afanikiwa kuifungia Juventus goli lake la kwanza baada ya kufunga magoli mawili na kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Sassuolo

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33, alicheza mechi 3 bila kufunga goli na ilimchukua dakika 5 tu za kipindi cha pili kuweza kupata goli hilo la kwanza

Goli lake la kwanza limekuja ikiwa ni shuti lake la 28 la kujaribu kupata goli katika michezo minne kwa ajili ya Juventus sawa ya michezo na mashuti aliyochukua msimu uliopita akiwa Real Madrid ili kupata goli lake la kwanza

Aidha, goli lake la leo la pili ni goli la kihistoria kwani ni goli lake la 400 katika michuano yote ya ligi akiwa amecheza michezo 517. Magoli 311 alifunga akiwa Real Madrid, 84 akiwa Manchester United na 3 akiwa Sporting Lisbon

0 comments:

Post a Comment