Nyota wa klabu ya Crystal Palace Wilfried Zaha amesema kwamba wapinzani huwa wanaingia uwanjani kumuumiza na anaomba Waamuzi wamlinde kama wachezaji wanaocheza vilabu vikubwa.
Zaha ameshachezewa rafu mara 11 msimu huu mpaka sasa baada ya mechi tano na sio mara ya kwanza kudai kwamba anaumizwa sana na rafu.
. “ sasa hivi najua kabisa wapinzani wanataka kuniumiza, tatizo sijui nifanye nini tena .”
“ Naishia kubishana na waamuzi tu, kwa mfano leo ( jana ) nilikuwa na bahati jamaa kanikanyaga kwenye ugoko ambapo kuna kinga , hivi inahitajika mpaka nivunjike mguu ndio mtu apewe kadi nyekundu ?
“ Wiki iliyopita dhidi ya Watford nilirukiwa kwenye kiazi cha mguu . Nifanye nini zaidi ili na mimi nilindwe kama wachezaji wengine .”
“ Sina kingine cha kufanya zaidi ya kuendelea kujituma na kucheza soka bila kupoteza utulivu wangu hata maumivu yakizidi.”
0 comments:
Post a Comment