Wednesday, December 12, 2018

Timu ya Simba imefanya mazoezi kwenye mji wa Kitwe, Zambia kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Nkana FC.

Haji Manara amesema kila kitu kipo sawa na wamepata mapokezi mazuri kutoka kwa klabu ya Nkana.

"Timu imefika salama katika mji wa Kitwe mida ya saa 8 kasoro, wachezaji wako vizuri na tumepata mapokezi mazuri kutoka kwa klabu ya Nkana na kila kitu kina kwenda vizuri"-Afisa habari Simba SC.

"Tunasubiri kwa hamu game ya Jumamosi hapa Kitwe-Zambia na tumejipanga kikamilifu, Inshaallah itakuwa."

Simba na Nkana zitacheza mchezo wa kwanza siku ya Jumamosi December 15, 2018.

0 comments:

Post a Comment