Miamba hao wa Catalan wataikabili Real Madrid Jumamosi wakiwa wanaongoza kwa pengo la alama 11 dhidi ya mahasimu wao wakuu kwenye msimamo wa ligi.
Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta amesisitiza kuwa timu yake itakuwa na kibarua kizito katika mbio zao za taji la La Liga ikiwa wanataka kupata matokeo chanya kwenye uwanja wa Bernabeu wikiendi ijayo.
Miamba hao wa Catalan wataikabili Real Madrid Jumamosi wakiwa wanaongoza kwa pengo la alama 11 dhidi ya mahasimu wao wakuu kwenye msimamo wa ligi.
Atletico Madrid wakizidiwa pointi sita na Barca, lakini Valencia wameachwa pointi nane, jambo ambalo Iniesta anaamini ni pengo dogo sana kujifariji kuelekea mechi ya kwanza ya El Clasico msimu huu.
Alipoulizwa kama Real Madrid wapo nje ya mbio hizo tayari ikiwa watafungwa, aliwaambia waandishi: "Kusema ukweli, sidhani. Ni vigumu kusema kuwa La Liga itakuwa imekwisha ifikapo mwezi Desemba.
"Ni kweli kwamba kama tukifanikiwa kuwafunga tutakuwa tumepiga hatua kubwa, lakini hatuwezi kuisahau Atletico Madrid, ambayo tumeizidi alama sita tu. Tunatazamia kucheza soka bora na kujaribu kuondoka na pointi tatu."
Barcelona wamepoteza pointi katika mechi tatu tu kwenye mechi 16 za msimu huu, Ernesto Valverde akiwa hajaonja kipigo tangu achukue mikoba ya Barca.
0 comments:
Post a Comment