Nigeria huenda sio wanaopigiwa upatu kushinda kombe la dunia lakini wanaonekana kupata mashabiki wengi kupitia jezi yao mpya.
Mashabiki milioni 3 tayari wameagiza tisheti kama hizo kulingana na shikisho la soka la Nigeria na wanunuzi walipanga foleni nje ya duka la kampuni ya jezi ya Nike mjini London siku ya Ijumaa ili kujaribu kununua nguo hizo.
Tisheti hizo zilizokuwa zinauzwa kwa bei ya £64.95, ziliuzwa katika tovuti ya kampuni ya Nike muda mfupi baada ya kutolewa.
Kiungo wa kati wa Arsenal Alex Iwobi ni miongoni mwa waliouza jezi hizo ambazo zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Februari , pamoja na mchezaji wa Leicester Wilfried Ndidi, ambaye alivaa kofia na jaketi katika picha za kampeni ya kuziuza jezi hizo.
Nigeria imevaa kwa mara ya kwanza jezi hizo leo kwenye mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya uingereza na mchezo huo umeisha kwa kufungwa goli mbili bila magoli yakitiwa nyavuni na cahil pamoja na kane.
0 comments:
Post a Comment